ARUSHA;Rais John Magufuli jana,alitua kwa mara yakwanza katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro tangu aingie madarakan na kuwataka wakazi wake kufanya kazi,kwani uchaguzi umekwisha.
Akizungumza na mamia ya watu waliojitokeza kumpokea katika uwanja wa ndege wakimataifa wa Kilimanjaro(KIA)na barabara kuu ya Arusha-Moshi,DK MAGUFULI alishukuru kwa mapokezi aliyo yapata na kusema hata waangusha wananchi hao.
"Uchaguzi umekwisha ndugu zangu sasa ni kazi tu na wananchi wa Arusha na Kilimanjaro sitawaangusha ahadi zangu zote nlizo waahidi wakati wa kampeni nitazitekeleza"Alisema.
Alisema anajua matatizo ya Arusha na Kilimajaro na kama alivyo ahidi atatekeleza yote.
Katika uwanja wa KIA Dk Magufuli alipokelewa na viongozi wa serikali wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Arusha,FILEX MTIBANDA,mkuu wa mkoa wa kilimanjaro,AMOS MAKALA pamoja na wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Arusha,wenyekiti wa almashauri na baadhi ya wabunge.
Comentarios