RIHANA NA KANYE WEST WATOA ALBAMU MPYA..

Ni miaka mitano tangu nyota wamuziki  Rihhana atangaze anaanda albamu yake mpya.

Hataivyo harakati hizo zilikabiliana na changamoto chungu nzima na kulazimika kuchelewesha utayarishaji wake.

Lakini hatimaye ndoto yake imefaulu na sasa albamu hiyo ya nane kwa jina la ANTI imekamilika.

Nyota huyo alifanya tangazo hilo akiwa amevaa taji la dhahabu la malkia pamoja na vipaza sauti vya masikioni vya dolce na gabbana.

Wakati huohuo albamu ya nyota Kanye west'SWISH'ilitarajiwa kuwa tayari kwa onyesho lake la Glastonbury wakati wa msimu wa joto ulio pita.

Hatahivyo mpango huo haukufaulu huku nyota huyo wa muziki wa rap akiambia vanity fair kwamba alikua anaichelewesha kwa makusudi.

Lakini usiku wa jana alitangaza kwamba albamu hiyo iko tayari.

Comentarios