waumini wengi wa kianglikana nchini uingereza wanaunga ndoa za wapenzi wa jinsia moja,kulingana na kura za maoni.
Kati ya zaidi ya waanglikana 1,500 walihojiwa asilimia 45 ilisema kuwa ndoa za wapenzi wa jinsia moja zinafaa kuendelea huku asilimia 37 ikasema kuwa ni makosa.
Kura hiyo ya maamuzi ya Yougov pia imesema kuwa kunaongezeko la waumini wa kanisa hilo wanaunga ndoa za jinsia moja katika kipindi cha miaka mitatu iliyo pita.
Msimamo rasmi wa kanisa la uingereza kwamba ndoa inaweza kuwa ya mume na mke pekee.
Miaka mitatu iliyo pita ,kura kama hiyo ya Yougovu ilibaini kuwa asilimia 38 ya waanglikana wanaunga mkono ndoa za hizo huku asilimia 47 wakipinga.
Comentarios