Ndege yakubeba abiria imetua kwa dharura katika uwanja wa ndege mjini Mogadishu,Somalia ikiwa na shimo kubwa kwenye kiunzi chake.
Shimo hilo kwenye ndege hiyo lilitoboka mdamfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka Mogadishu,ikiwa futi 10,000(3,048)juu angani,jamaa wa mmoja wa abiria amewaambia waandishi.
Haijabainika ni nini kilicho toboa shimo hilo.
Maafisa wanasema abiria wawili waliumia.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Daallo,iliyokua ikielekea Djibouti,ilikua imebeba watu karibu 60,afisa wa polisi ameambia shirika la habari la Bloomberg.
Baadhi ya ripoti zinasema ndege hiyo ilishika moto muda mfupi baada ya kupaa.
Darren Howe,ambaye mwenzake alikua ameabiri ndege hiyo,alipiga picha inayoonyesha shimo hilo muda mfupi baada ya ndege hiyo kutua.
'Hakukutokea mlipuko. Ni kiunzi cha ndege kilicho pata hitilafu ndege ikiwa futi 10,000 angani'ALISEMA ABIRIA.
Comentarios