Huyu ndiye Polisi mwanamziki, soma hapa..

BAHATI  KASAMBA INNOCENT

Kwa kawaida polisi huzingatiwa kuwa watu wenye kuwaandama wahalifu na kilawakati wanapoonekana, wengi hujiuliza kwani leo kulikoni?

Na hali huwa ni ya wasiwasi zaidi ikiwa mmoja wa maafisa hao wa polisi ni wa cheo cha juu.
Bahati Kasamba Innocent, ni afisa wa cheo cha juu ndani ya idara ya polisi nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo anayesifika sana katika fani ya uimbaji wa njimbo za Injili.
Anasema yeye huimba katika juhudi za kuhubiri amani, uongozi bora na upendo.

Mwaandishi wa habari mashariki mwa Jamuhuri  ya kidemokrasia ya Congo huko bukavu, alikutana na msanii huyo studioni akiandaa baadhi ya nyimbo zake.

Comentarios