Mwanamuziki MAURICE WHITE afariki dunia..

Mwanamuziki nyota wa nyimbo za mtindo wa soul Maurice White,aliyeanzisha kundi maarufu la  wanamuziki la Earth, wind and Fire miaka ya sitini amefariki dunia.

Alijulikana kwa vibao kama vile september, Boogie Wondersland, shinning star na After the love has Gone.

Amefariki akiwa na umri wa miaka 74 akiwa usingizini Los Angeles, kakake Verdine White amesema.

Kundi hilo lilimshirikisha kakake na pia mwanamuziki Philip Bailey.

Wanamuziki hao kwapamoja walichomoa vibao vilivyo vuma sana miaka ya sabini. 
Kwajumla, waliuza zaidi ya albamu milioni 90 kote duniani na kushinda tuzosita za Grammy.

Maurice White aliye julikana sana kama Reese, alijiondoa Earth Wind And Fire mwaka 1995.

Alifichua hadharani kwamba alikuwa akiugua ugonjwa wa kutetemeka 'parkinson' miaka mitano baadaye wakati bendi hiyo ilipokuwa ikiingizwa rasmi kwenye  Rock And Roll Hall of Fame.

White alifanya kazi kama produsa,  akifanya kazi na wanamuziki wengine maarufu kama vile Barbra streisand, cher na Diamond

Comentarios