Phiri wa Free State, Awa kocha mkuu Mbeya City..

Kocha phiri.

Katibu mkuu wa Mbeya city Emmanuel Kimbe amesema Phiri alitua jijini Mbeya jana jioni, na leo jioni anatarajia kuanza kazi kwa kushirikiana na watu wengine waliopo kwenye benchi la ufundi kwani meja mstaafu Abdul  Mingange kwasasa yupo mapumziko  kutokana na matatizo ya kifamilia yaliyo kua yakimkabili.

Kimbe amesema moja ya kazi ambazo Phiri anatakiwa kuzifanya ni kuhakikisha anaibakisha timu kwenye ligi kwani matokeo wanayo yapata  si mazuri kwao jambo analoamini  ni kwamba inawezekana kutokana na uwezo wake.

Phiri kinna amezaliwa miaka 61iliyopita jijini Blantyre Malawi ndiye aliye msajili Mrisho ngasa katika klabu ya Free State ya Afrika ya Kusini.

Comentarios