wachezaji wa timu ya taifa ya jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo wamezawadiwa magari ya kifahari baada ya kushinda kombe la taifa bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani(CHAN).
Rais JOSEPH KABILA amewatunuku kila mchezaji gari la kifahari la thamani ya $60,000.
Chui hao wa kinshasa walitwaa kombe kwa kulaza mali 3-0 kwenye fainali na kuwa taifa la kwanza kushinda kombe hilo mara mbili.
Mchezaji HERITIER LUVUMBU NZINGA aliyeumia kwenye michuano hiyo ameahidiwa kwamba atasafirishwa ng'ambo kwa matibabu.
Comentarios