Katika tamaduni nyingi kote duniani mwanamke anapoolewa
huwa ni fahari kubwa sana akiwa ni bikira.
Mathalan ni dhihirisho la mwanamke kuwa amelelewa na
kutunzwa vyema.
Ni dhihirisho la usafi.
Hata hivyo jamii moja nchini Malawi haithamini ubikira wa
watoto wao wa kike.
Amini usiamini wazazi huwa wanamlipa ''Fisi'' kumbikiri binti
yao punde tu anapopata hedhi yake ya kwanza.
Wanaamini kuwa binti ambaye ni bikira ni mkosi kwa jamii!
Malimwengu haya.
Wazazi na jamii kwa jumla katika maeneo mengi ya kusini
mwa Malawi wamekuwa wakishikilia tamaduni hii kwa miaka
na mikaka.
''Fisi'' ama wanaume wanaowabikiri watoto wa kike
huchaguliwa na wazazi kuwaondolea mikosi.
Na huwa ni sherehe kubwa inayomtangulia binti kupelekwa
unyagoni kisha kuwatembelea shangazi wake kabla ya
kujulishwa kwa fisi.
Amini usiamini hao mafisi hulipwa takriban dola $7 kwa kila
kitendo cha ngono na hao mabinti ambao wengi huwa na
kati ya umri wa miaka 11-14.
Fisi mmoja katika kijiji cha Nsanje, Eric Aniva ameiambia BBC
kuwa hajui kwa kweli amewabikiri wasichana wangapi, kwa
sababu ni wengi.
''Kwa kweli mimi nimewabikiri zaidi ya wasichana 104,"
amesema. ''Hii ndiyo tamaduni yetu''.
''Hapa mwanamke akifiwa lazima aje kwangu nimuondolee
mkosi hata kabla ya kuzikwa kwa mumewe''.
''Mwanamke akiavya mimba pia kabla hajarejelea maisha
yake ya kawaida ama hata kushiriki ngono na mwanamume
mwengine lazima aje kwangu nimsafishe," alisema fisi huyo.
Aniva ambaye ana umri wa takriban miaka 40 ana wanawake
wawili na watoto 5.
Anasema kuwa pale anaposhiriki ngono na watoto hao huwa
anapewa muda wa siku 3 hivi kumsafisha na kumuondolea
mkosi.
Kulingana na tamaduni zao, ikiwa mwanamke ama binti
anakataa asibikiriwe huwa wanaamini kuwa jamaa zao
watafuatwa na mikosi na magonjwa.
Comentarios