Mwanaye Osama aapa kulipiza mauaji ya babake

Mwanaye aliyekuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al
Qaeda Osama bin Laden, ameapa kulipiza kisasi kwa mauaji
ya babake.

Katika ujumbe wa sauti uliochapishwa katika mitandao
Hamza bin Laden ameapa kulipiza kisasi kwa Marekani kwa
kumuua babake 2011 huko Pakistan.
Ujumbe huo wa dakika 21 wenye kichwa "We Are All
Osama,", Hamza ambaye inaaminika kuwa alikuwa na babake
makomando wa Marekani walipowavamia na kumtwaa
ameapa kuendeleza kazi aliyoianza babake.

''Tutaendelea kuwasaka na kuwapiga popote pale
mtakapokuwa mumejificha ati nyuma ya pazia za usalama
kwa maovu munayoyaendeleza ,Palestina, Afghanistan, Syria,
Iraq, Yemen, Somalia na kote kwenye ardhi ya waislamu
mnayokalia '' shirika la habari la Reuters linamnukuu.

''na kwa wale wanaodhania kuwa tutakuwa tukilipiza kisasi
mauaji ya Osma ole wenu, kwanini sisi tutakuwa tukilinda
dinia ya kiislamu'' alisema Hamza.
Osama aliuawa na makomando wa marekani katika maficho
yake huko Pakistan mwaka wa 2011.

Hamza ambaye kwa sasa ana umri wa kati ya miaka ishirini
hivi alikuwa na babake kabla ya mashambulizi ya kigaidi ya
mwaka wa 9/2001 huko Afghanistan kabla ya kukimbilia
Pakistan kufuatia mashambulizi makali ya Marekani na
washirika wake.

Hamza kulingana na wachanganuzi anatambulishwa na
kiongozi wa kidini wa kundi hilo Ayman al-Zawahiri katika
ujumbe huo unaolenga kuwavutia vijana ambao kwa sasa
wamejiunga kwa wingi na kundi la Islamic state.

Comentarios