Wanawake waislamu nchini Rwanda,wapigwa marufuku
wasijifunike nyuso zao.
Hatua hiii imechukuliwa na jumuiya ya waislamu nchini humo
iliyofikia uamuzi wa kuipiga marufuku vazi hilo la Niqab
linalovaliwa na wanawake.
Vazi hilo hufunika uso wote wa mwanamke.
Jumuiya hiyo imesema marufuku hiyo inatokana na sababu
za kiusalama kwa waislamu na vilevile warwanda.
'' Hili vazi ni la kiislamu hata hivyo limeanza kutumika vibaya
kwa madhumuni ya kudhuru usalama wa waisilamu na
vitendo vinavyokinzana na mafunzi ya dini ya Kiislamu''
''Jambo la pili ni usalama wa nchi. kwa sababu watu
wanajificha na kutenda vitendo pasi na kutaka kuonekana''.
''Tumeona fikira potofu tayari ikifuja na ndiposa tukachukua
uamuzi huu kuzuia kuenea kwa uovu'' alisema sheikh Mussa
Sindayigaya.
Uamuzi huo umetokea wakati kundi la watu 17 wa kiislam
wanazuiliwa nchini humo kwa tuhuma za kutaka kujiunga na
kundi la IS na kufundisha itikadi za kundi hilo.
Katika msikiti mkuu wa Nyamirambo jijini Kigali ni wakati wa
swala ya adhuhuri,,,waislam wengi wanaingia msikitini …
lakini huwezi kuona hata mmoja anayevaa niqab miongoni
mwa wanawake au mabinti wanaoingia hapa msikitini
Wanawoiunga mkono kauli hiyo ya jumuiya ya waislam nchini
Rwanda wanasema kuwa Niqab ilikuwa imeanza kutumika
kuficha maoavu mengi katika jamii.
Aidha wanasema kuwa wanawake waislamu wanapaswa
kuwajibika kwa kujiepusha na maovu ambayo sasa yameanza
kuchipuka kwa kisingizio cha Niqab.
Kuna wengine walioghadhabishwa na uamuzi huo lakini
hawakutaka kuzungumzia suala hilo wakisema wanahofia
usalama wao.
Hapo nyuma kundi la waislam zaidi ya 17 lilishikwa na
kufunguliwa mashtaka ya kusajili vijana wa kujiunga na kundi
la Islamic State na pia kueneza itikadi za
Comentarios