Rais wa Nicaragua Daniel Ortega amemtaja mkewe kama
mgombea mwenza na makamu wa rais wakati huu ambapo
anawania kuchaguliwa kwa muhula mwengine.
Mkewe Rosario Murillo tayari ana wadhfa maarufu wa
msemaji wa serikali na anaonekana kuwa anagawana
mamlaka na mumewe.
Amekuwa akionekana katika runinga ya Nicaragua kila siku
Wakosoaji wanawashtumu wanandoa hao wawili kwa
kuiendesha Nicaragua ambayo inakabiliwa na uchaguzi mkuu
mwezi Novemba kama chombo chao cha kibinafsi.
Rais Ortega akiwa hazungumzi sana katika vyombo vya
habari ,mkewe huonekana mara kwa mara katika runinga
akijadili sera na kujikuza .
Akiwa mama wa watoto 7 wa rais huyo anajua kuongea
Kiingereza na Kifaransa huku akijulikana pia kuwa mshairi.
Pia anasifa za kuvaa mavazi yenye rangi nyingi na vito vya
miaka ya sitini.
Wanahabari wanasema kuwa raia wengi wa taifa hilo
wanamuona bi Murillo kama mwenye uwezo mkubwa katika
taifa lake kutokana na hadhi yake katika uma.
Mume na mkewe waliwasilisha makaratasi yao ya kugombea
viti hivyo rasmi katika mji mkuu wa Managua wakiandamana
na mshauri wakili wa chama chao cha Sandinista.
Comentarios